Afrika yatangaza dharura ya kiafya ya mripuko wa mpox
13 Agosti 2024Matangazo
Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa barani Afrika, Africa CDC, leo kimetangaza dharura ya kiafya kutokana na mripuko wa homa ya nyani katika bara hilo.
Tangazo hilo limetolewa na mkuu wa kituo hicho Jean Kaseya katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwa njia ya mtandao. Kulingana na takwimu za CDC, kufikia Agosti 4, kulikuwa na zaidi ya visa 38,000 vya homa ya nyani na vifo zaidi ya 1,400 barani Afrika tangu Januari mwaka 2022. Kaseya amesema tangazo hilo ni wito wa hatua kuchukuliwa ili kukiangamiza kitisho kinachotokana na homa hiyo.