Afrika mashariki itapoteza sifa kuwa chimbuko la binadamu?
30 Novemba 2018Wataalamu wa utafiti wa mambo ya kale nchini Algeria, wamegundua zana zilizotengenezwa kwa mawe na mifupa ya wanyama iliokatwa ambayo huenda vina umri wa hadi miaka milioni 2 na laki 4, na hivyo kusababisha utata juu ya eneo la Afrika mashariki kuwa chimbuko la binadamu.
Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa Alhamisi na jarida la Sayansi ugunduzi huo umetokea katika Setif kilomita zipatazo 300 mashariki mwa mji mkuu Algiers, kutokana na utafiti wa kikudi cha wataalamu wa kimataifa wakiwemo kutoka Algeria.
Vifaa hivyo vinafanana na vile vinavyoitwa Oldwan, vilivyogunduliwa Afrika Mashariki.
Wataalamu wanaashiria kwamba watangulizi wa binadamu wa leo waliishi Afrika kaskazini kwa karibu miaka 600,000 kabla kuliko ilivyokuwa ikidhaniwa na wanasayansi.