Matangazo
Mabadiliko ya tabia nchi yanatishia sio tu kuongezeka kwa majanga ya asili kama vile mafuriko, ukame, joto kali na vimbunga bali pia yanatishia afya za watu hasa watoto. Kwa mujibu wa ripoti ya Lancet ya mwaka huu wa 2019, hali huenda ikawa mbaya zaidi endapo hatua madhubuti hazitochukuliwa. Katika makala ya Mtu na Mazingira, tunaangazia athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa afya ya binadamu na kilimo. Ungana na Babu Abdalla kwa mengi zaidi.