Azerbaijan yashtumu mataifa ya Magharibi kwa kuiharibia sifa
12 Novemba 2024Akihutubia mkutano huo wa COP29 mjini Baku, Rais Aliyev, amesema wale wanaosema uchumi wa taifa lake unategemea zaidi uchimbaji na usafirishaji wa mafuta au gesi asilia, wanaonyesha ukosefu wa ufahamu.
Rais Aliyev ameongeza kuwa ilikuwa sawa kusema hivyo katika karne ya 19, wakati nchi hiyo ilichangia zaidi ya nusu ya uzalishaji wa mafuta duniani, lakini kusema hivyo sasa kunaonesha tu ukosefu wa utamaduni wa kisiasa na ufahamu.
Aliyev asema akiba ya mafuta na gesi ya Azerbaijan ni "zawadi ya Mungu"
Aliyev alirejelea mtazamo wake unaoibuwa utata kwamba akiba ya mafuta na gesi ya Azerbaijan ni "zawadi ya Mungu" na nchi hazipaswi kulaumiwa kwa kuzimiliki na pia hazipaswi kulaumiwa kwa kuleta rasilimali hizo sokoni kwa sababu soko linazihitaji, na wananchi wanazihitaji.
Mkutano wa kilele wa mazingira COP29 waanza Azerbaijan
Kwenye mkutano huo wa COP29 mjini Baku waziri mkuu wa Uingereza Keir Starmer nae ameahidi kuchukua hatua kubwa zaidi kufikia lengo la nchi yake la kupunguza gesi inayochafuwa mazingira akisema uzalishaji wa gesi chafuzi utapunguzwa kwa asilimia 81 ikilinganishwa na viwango vya 1990 ifikapo mwaka 2035 huku serikali yake ikiimarisha azma yake juu ya mabadiliko ya tabianchi.
Mahakama ya rufaa ya Uholanzi yabatilisha uamuzi dhidi ya kampuni ya mafuta ya Shell
Wakati wajumbe wakijadili kuhusu hatua za kuchukuliwa kuuokowa ulimwengu na mabadiliko ya tabia nchi mjini Baku, mahakama ya rufaa nchini Uholanzi leo imebatilisha uamuzi wa kihistoria ulioiamuru kampuni ya mafuta ya Shell kupunguza uzalishaji wake wa hewa chafu ya kaboni kwa asilimia 45 ifikapo mwaka 2030 ikilinganishwa na viwango vya mwaka 2019, huku ikisema kwamba ulinzi dhidi ya mabadiliko hatari ya tabianchi ni haki ya kibinadamu.
Uamuzi huo ni pigo kwa tawi la Uholanzi la mtandao wa kimataifa wa mashirika ya mashinani ya harakati za kulinda kimazingira katika nchi 73 Friends of the Earth, pamoja na makundi mengine ya kimazingira ambayo yalisifu uamuzi wa awali wa mwaka 2021 walioutaja kuwa ushindi kwa mazingira.
Guterres: Athari za mabadiliko ya tabia nchi ni kubwa
Mkuu wa Friends of the Earth nchini Uholanzi Donald Pols, amesema uamzi huo unaumiza. Amesema kesi hiyo imeonesha kwamba makampuni wachafuzi wakubwa wa mazingira yanaweza pia kuchukuliwa hatua lakini pia kesi hiyo imechochea zaidi mjadala kuhusu wajibu wao katika kupambana na mabadiliko hatari ya tabianchi.
Guterres: Tuendelee kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
Uamuzi huo pia uliashiria kushindwa pakubwa kwa wanaharakati wa kutetea mazingira baada ya ushindi kadhaa mahakamani. Mnamo mwaka 2015, mahakama ya The Hague iliiamuru serikali ya Uholanzi kupunguza uzalishaji wahewa chafuzi kwa angalau asilimia 25 ifikikapo mwishoni mwa mwaka 2020, kwa kuzingatia viwango vya 1990.