SiasaAsia
Bangladesh kuunda serikali mpya ya mpito
8 Agosti 2024Matangazo
Serikali hiyo iliyopewa jina la "serikali ya washauri" inatazamiwa kuapishwa wakati wowote kuanzia sasa.
Yunus, mwenye umri wa miaka 84, amependekezwa kuchukuwa nafasi hiyo na wanafunzi wenyewe, walioongoza vuguvugu la kumpinduwa Hasina.
Soma zaidi: Rais wa mpito wa Bangladesh kuapishwa Alhamis
Mchumi huyo ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa Hasina, anatazamiwa kuwasili mjini Dhaka akitokea Paris alikokuwa kwenye matibabu.
Licha ya umri wake mkubwa, viongozi wa wanafunzi na makundi mengine ya wanaharakati wanaamini kuwa ndiye mtu anayefaa kuiongoza Bangladesh kuelekea uchaguzi mkuu, na kuondosha uwezekano wa taifa hilo la kusini mwa Asia kuangukia mikononi mwa jeshi.