Baraza la Usalama kuiondolea Somalia vikwazo vya silaha
1 Desemba 2023Haya yamesemwa na wanadiplomasia, zaidi ya miaka 30 baada ya nchi hiyo kuwekewa vikwazo vya kununua silaha. Baraza hilo la usalama lenye wanachama 15 katika kura hiyo linatarajiwa kukubali rasimu mbili za maazimio zilizoandikwa na Uingereza.
Mojawapo ya rasimu hizo ni ya kuondoa kikamilifu vikwazo vya silaha ilivyowekewa Somalia na nyengine ni ya kuliwekea vikwazo vya silaha kundi la kigaidi la Al Shabaab lililo na mafungamano na mtandao wa Al Qaeda.
Soma pia: Somalia karibu Kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki
Baraza hilo la usalama liliiwekea serikali ya Somalia vikwazo mwaka 1992 ili kukata usambazaji wa silaha kwa wababe wa kivita waliokuwa wamempindua dikteta Mohamed Siad Barre na kuitumbukiza nchi hiyo ya Pembe ya Afrika katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.