MigogoroSudan
Umoja wa Mataifa kujadili kusitishwa uhasama nchini Sudan
18 Novemba 2024Matangazo
Muswada huo ulioandaliwa na Uingereza na Sierra Leone, unatoa wito kwa wahusika "kusitisha uhasama mara moja na kushiriki kwa nia njema katika mazungumzo ya amani ili hatimaye kufikiwa mpango wa usitishwaji mapigano.
Sudan imeharibiwa na vita tangu Aprili mwaka 2023 kufuatia mapigano kati ya jeshi la la Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ambaye alichukua madaraka katika mapinduzi ya mwaka 2021.
Kikosi cha RSF kinaongozwa na naibu wake wa zamani, Jenerali Mohamed Hamdan Daglo.