Bei ya mafuta nchini Zimbabwe yapanda mara mbili
24 Juni 2020Bei ya mafuta nchini Zimbabwe zitapanda kwa hadi asilimia 152 leo, idara ya udhibiti wa bei za nishati imesema, baada ya serikali kuondoa kiwango maalum kilichowekwa tangu mwezi Machi.
Mara ya mwisho nchi hiyo ya kusini mwa Afrika iliposhuhudia ongezeko la juu la bei la mafuta, Januari mwaka 2019, kulizuka maandamano yaliyokuwa na ghasia, na kusababisha zaidi ya watu 17 kuuwawa baada ya ukandamizaji uliofanywa na majeshi ya usalama.
Zimbabwe tayari inapitia mzozo mbaya kabisa wa kiuchumi katika muongo mmoja , kukiwa na ughali wa maisha wa kiwango cha juu, na ukosefu wa dawa na chakula. Bei ya mafuta itapanda kwa dola za Zimbabwe 71.62 sawa na dola za Marekani 1.25 kwa lita, kutoka dola ya Zimbabwe 28.96.