Biden airuhusu Ukraine kutumia makombora ya masafa marefu
18 Novemba 2024Hayo yamesemwa na afisa wa Marekani aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, na hivyo kuthibitisha taarifa zilizochapishwa na vyombo vya habari vya Marekani na ambayo inaashiria mabadiliko makubwa ya sera.
Hatua hiyo iliyokuwa ikitakiwa kwa muda mrefu na Kiev, imechukuliwa saa chache baada ya Urusi kufanya mashambulizi makubwa yaliyolenga gridi ya umeme ya Ukraine, na pia ni jibu kwa kitendo cha Korea Kaskazini kupeleka wanajeshi Moscow.
Hata hivyo, bado kitendo cha kurejea kwa Donald Trump katika Ikulu ya White House januari mwakani kinaendelea kuzusha hofu kuhusu mustakabali wa uungaji mkono wa Marekani kwa Kyiv.
Urusi yafanya mashambulizi makubwa Ukraine
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema Urusi imeshambulia nchi yake kwa makombora 120 na ndege 90 zisizo na rubani 90 siku ya Jumapili.
Mashambulizi hayo makubwa yalilenga miundombinu ya nishati ya nchi hiyo. Rais Zelensky amesema vikosi vya ulinzi vya Ukraine vilifaulu kuangusha makombora 140 ya angani lakini kuna uharibifu uliofanyika.
Soma pia: Nchi za G7 zasisitiza kuendelea kuiunga mkono Ukraine
Ameendelea kuwa katika mji wa Mykolaiv, mashambulizi ya ndege zisizo na rubani yamesababisha vifo vya watu wawili. Watu wengine sita wamejeruhiwa, wakiwemo watoto wawili. Mkuu wa kijeshi wa jiji la Kiyv Serhii Popko amesema mashambulizi hayo mapya ya urusi ya ndege zisizo na rubani na makombora yalikuwa ni makubwa zaidi.
(Vyanzo: AP, DPAE, AFP)