Bodi ya IAEA yailaani Iran kwa kushindwa kutoa ushirikiano
22 Novemba 2024Shirika hilo pia, limeitaka Iran itoe majibu katika uchunguzi wa muda mrefu unaohusu kupatikana kwa chembe chembe za urani katika maeneo mawili ambayo nchi hiyo imeshindwa kuyatangaza kuwa maalumu kwa kuzalisha nyuklia.
Soma zaidi: IAEA: Iran yapanua uwezo wa kurutubisha madini ya urani
Kwa mujibu wa wajumbe waliozungumza kwa sharti la kutotajwa majina, wanachama kumi na tisa wa bodi hiyo ya IAEA walipiga kura kuunga mkono azimio la kuilaani Iran, huku Urusi, China na Burkina Faso zikilipinga. Mataifa 12 yalijizuia kushiriki na moja likikosa kupiga kura hiyo.
Azimio hilo liliwasilishwa na Ufaransa, Ujerumani na Uingereza na kuungwa mkono na Marekani. Katika taarifa baada ya kupitishwa kwa azimio hilo, Iran ililaani hatua hiyo na kusema inachukuwa hatua mwafaka za kurutubisha madini ya urani.