BOGOTA: Bush amekabiliwa na maandamano ziarani
12 Machi 2007Rais George W.Bush wa Marekani amewasili mji mkuu wa Colombia,Bogota akiwa katika kituo cha tatu cha ziara yake ya mataifa matano barani Amerika ya Kusini.Alipokutana na rais wa Colombia Alvaro Uribe ambae ni mshirika wake mkuu katika bara hilo,Bush aliahidi kuisaidia nchi hiyo kupiga vita kilimo cha madawa ya kulevya na vile vile kupambana na waasi wa chama cha FARC cha mrengo wa shoto.Kwa upande mwingine,wafanya maandamano walichoma moto bendera za Marekani na walipambana na polisi,kabla ya maandamano hayo kuvunjwa.Hadi polisi na wanajeshi 22,000 walitawanywa katika mji mkuu Bogota kwa ziara hiyo fupi ya Bush,baada ya ziara zake nchini Brazil na Uruguay kukabiliana na maandamano.Ziara hii ya Bush inampeleka Guatemala na Mexico ambako pia inahofiwa kuwa yatakuwepo maandamano ya kumpinga Bush.